Posts

Showing posts from November, 2023

SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI NA KULAKIWA NA DKT. CHANA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakikagua gwaride la heshima, tarehe 23 Novemba, 2023 mara baada ya kuwasili nchini. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit mara baada ya kuwasili nchini, tarehe 23 Novemba, 2023 Jijini Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit amewasili nchini tarehe 23/11/2023 na kupokewa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kushiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha. Mara ya mwisho Rais Salva Kiir kuja nchini ilikuwa April 15, 2016 ambapo alikutana na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unahudhuriwa

WAZIRI CHANA ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akishiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 22 Novemba, 2023 Jijini Arusha. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akishiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 22 Novemba, 2023 Jijini Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana anashiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyikia Jijini Arusha. Mkutano huo ulioanzia katika Ngazi ya Wataalam waliokutana Jijini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2023 na ukafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 21 Novemba 2023, kinakamilishwa na Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri ulioanza leo tarehe 22 Novemba 2023. Masuala yanayojadiliwa katika Mkutano huo wa wataalam ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Maw

DKT. CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SINGAPORE NCHINI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akifanya mazungumzo na Balozi wa Singapore nchini Mhe. Douglas Foo,  tarehe 20 Novemba, 2023 mtumba, Jijini  Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikabidhi Balozi wa Singapore nchini Mhe. Douglas Foo mfuko maalum ambao ni rafiki wa mazingira unaotumika kwenye “Mama Samia Legal Aid Campaign” tarehe 20 Novemba, 2023  Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Singapore nchini Mhe. Douglas Foo kwenye picha ya pamoja na washiriki kwenye kikao kilichowakutanisha viongozi hao wawili, tarehe 20 Novemba, 2023 Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Balozi wa nchi ya Singapore nchini Mhe. Balozi Douglas Foo na kufanya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali na namna ya kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya teknolojia. Kikao hicho kimefanyika t

KASI YA UJENZI IENDANE NA UBORA: DKT. CHANA

Image
Mhandisi Nassiri Nassoro akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana, tarehe 17 Novemba, 2023 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara, tarehe 17 Novemba, 2023   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara ambao umefikia asilimia 79 linaojengwa Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, na kumtaka Mkandarasi kuongeza kasi huku akizingatia ubora. Ukaguzi huo ameufanya tarehe 17 Novemba, 2023. “Kwenye ujenzi wa majengo haya tunashindana hivyo ukiona mwenzio ameweka vioo nawe unajiuliza la kwangu linawekwa vioo lini,” alisema Dkt. Chana huku akitahadharisha pamoja na mambo mengine upatikanaji wa maji kwenye jengo akitaka kuwepo na uwiano wa idadi ya watumishi na uwezo wa pampu ya kusukumuia maji ili yafike kwenye sakafu zote za jin

MHE CHANA AFANYA KIKAO NA MENEJIMENTI YA WIZARA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akiongea na menejimenti kwenye kikao kilichofanyika Mtumba, leo tarehe 16 Novemba 2023 jijini Dodoma.  Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa kwenye kikao cha utekelezaji wa majukumu ya Wizara leo tarehe 16 Novemba 2023. Mtumba jijini Dodoma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe - WKS – Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya kikao na Menejimenti ya Wizara pamoja na watalaam wa sheria kujadili mambo mbalimbali yakiwemo utekelezaji wa   mapendekezo ya haki jinai kwa   Wizara ya katiba na Sheria   pamoja na wasilisho la kutungwa kwa sheria ya kupinga ukatili   wa kijinsia yam waka   2023.   Kikao hicho ambacho kimefanyika leo tarehe 16 Novemba, 2023 katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma, Mhe. Chana amesisitiza watumishi kuhakikisha utekelezajiwa majukumu yaliyoamuliwa yanafanyika kwa ubunifu huku wakizingatia muda.  

MHE. CHANA ATEMBELEA KITUO JUMUISHI CHA MASUALA YA FAMILIA.

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja na badhi ya watumishi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, tarehe 15 Novemba 2023.   Naibu Msajili Mfawidhi Kituo Jumuishi Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Frank Moshi akimpa maelezo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana alipotembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, 15 Novemba, 2023 Jijini Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, tarehe 15 November 2023 ametembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke kukagua shughuli mbalimbali za kiutendaji. Akiwa Kituoni hapo Waziri Chana amepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Chumba maalumu ambacho kimetengwa kwa ajili ya akina mama kunyonyesha watoto wachanga wanapofika katika Kituo hicho kupata huduma.

CHANA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MASHUJAA WA VITA YA KWANZA YA DUNIA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi  Chana , Balozi Wa Uingerza nchini  David Concar  na Balozi wa Ujerumani  Nchini  Wakitoa  heshima  zao kwenye moja ya kaburi la mashujaa waliotoa uhai wao kwenye vita ya kwanza  ya  Dunia. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi  Chana , Balozi Wa Uingerza nchini  David Concar  na Balozi wa Ujerumani  Nchini  Wakitoa  heshima  zao kwenye moja ya kaburi la mashujaa waliotoa uhai wao kwenye vita ya kwanza  ya  Dunia XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku - WKS DSM Waziri wa Katiba n Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana Leo 12/11/2023 ameshiriki Ibada ya maadhimisho ya siku ya Mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita ya kwanza ya Dunia iliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya ya Madola Kijitonyama Jijini Dar es salaam. Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ubalozi wa Uingereza na Ubalozi wa Ujerumani Waziri Chana amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea   kuhamasisha Jamii na

WAZIRI CHANA AIPONGEZA NMB KWA KUTOA HUDUMA ZINAZOIGUSA JAMII

Image
  Waziri wa Katiba na  Sheria  Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na  Wanasheria Binafsi katika mkutano uliofanyika leo tarehe 10 Novemba Jijini Dar es Salaam . Waziri wa Katiba na  Sheria  Mhe Balozi Dkt Pindi Chanaajiongea na   Wanasheria Binafsi kwenye  mkutano uliofanyika leo tarehe 10 Novemba Jijini Dar es Salaam . Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Balozi   Dkt Pindi Chana  akipokelewa na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB kwenye mkutano wa NMB na Taasisi za Sheria Mkoa wa Dar es salaam.  Waziri wa Katiba naSheria  akiongoza na Mhe Omary Said Shabani  Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar  baada ya Kuwali kwenye Mkutano wa NMB  na Taasisi  za Sheria  Mkoa wa Dar es Salaam.  Na Lusajo Mwakabuku – WKS Waziri wa Katiba n Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana Ameshiriki Mkutano wa NMB na Taasisi za Sheria za Mkoa wa Dar es Salaam na Kuipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kufanya kazi kwa Weledi na kuiomba kuendelea kushiriki kwenye Huduma mbali mbali zinazogusa j

MHE CHANA ASHIRIKI MKUTANO WA TANZANIA - RUSSIA ALUMNI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiongea  kwenye mkutano wa Tanzania - Russia  Alumni ulifanyika  leo tarehe 08 Novemba 2023 jijini Dar es salaam.  Waziri wa katika na Sheria  Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana  akiongea na Afisa kutoka ubalozi wa Urusi nchini kweny mkutano  wa Tanzania - Russia Alumni ulifanyika leo tarehe 08 novemba  2023 jijini  Dar es salaam. Baadhi wa  watanzania waliosoma nchini Urusi wakiwa kwenye kikao cha Tanzania -Russia Alumni kilichofanyika  Dar es  salaam leo  tarehe 08 Novemba 2023.                           XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi Dkt.  Pindi Chana ameshiriki Mkutano wa Wanafunzi waliohitimu Vyuo vikuu vya Nchini Urusi uliofanyika Leo November 08, 2023 jijini Dar es salaam. Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Chana ameipongeza Urusi kwa kuendeleza ushirikiano mzuri na Vyuo vya Tanzania katika Kuboresha Elimu na kuwakaribisha zaidi kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama. Aidha,k
Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akitoa ufafanuzi kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 07 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akitoa ufafanuzi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 07 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora tarehe 07 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe - WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume za Haki za Binadamu na Utawala bora kwenye Kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria. Katika taarifa hiyo Mhe. Chana amefafanua kuwa utekelezaji wa majukumu ya Tume ni ya mtambuka kwani yanagusa maisha ya binadamu ya kila siku

MAHAKAMA YA MWANZO YA TARAFA YA BWAKILA CHINI KUJENGWA – MHE GEKUL

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akijibu swali Bungeni leo tarehe 07 Novemba 2023, Bungeni Jijini Dodoma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe- WKS – Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amefafanua kuwa Serikali katika mwaka fedha 2023/ 2034 imejipanga kujenga Mahakama zaidi ya 60 nchini na katika idadi hiyo pia ipo mahakama ya mwanzo ya tarafa ya Bwakila chini. Mhe Gekul ameyasema hayo leo tarehe 07/11/2023 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Morogoro Kusini Mhe Innocent Edward Kalongoles alitetaka kujua ujenzi wa mahakama katika eneo hilo utafanyika lini. Mhe Gekul amefafanua kuwa tayari zabuni imetangazwa kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mahakama hiyo na wakati wowote atatangazwa na kuanza kazi. Aidha, Mhe Gekul ameleza kuwa Mahakama ya mwanzo ya Matombo na Namvua zina majengo ya ambayo ni chakavu na tayari Serikali imeyaweka katika mpango wa ukarabati katika mwaka wa fedha 2024/2

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria leo tarehe 6 Novemba 2023 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akitoa ufafanuzi wa Jambo alipkuwa akiongea na    watumishi wa Wizara ya katiba na sheria leo 6 Novemba 2023 jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiongea na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria   leo tarehe 6 Novemba 2023 Jijini Dodoma. Watumishi wa Wizara ya Katiba wakimsikiliza waziri alipokuwa akiongea kwenye kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 6 Novemba 2023 mtumba jijini Dodoma XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. George Mwakyembe – WKS – Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amewataka watumishi pamoja na menejimenti ya Wizara yake kufanya kazi kwa kujituma, uadilifu na kwa ushirikiano ili kutimiza malengo ya Wizara katika kuwahudumia watanzania. Waziri Chana ameyase

SISI TUNA UHITAJI LAKINI WATOTO HAWA WANA UHITAJI ZAIDI: MAKONDO

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo na watumishi wa Wizara kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Safina Street Network, tarehe 04 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Bi. Esther Mwamukonda kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akikabidhi vitu kwa Mratibu wa Kituo cha Safina Street Network Bw. Ebenezer Eliawira Ayo, tarehe 04 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Safina Street Network kilichopo maeneo ya Ntyuka wakipata chakula walichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, tarehe 04 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amesema Watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi hapa nchini wana uhitaji mkubwa na changamoto nyingi kulinganisha na watu wengine, na kutoa wito kwa jamii kuendelea kuwakumbuka watoto hao mara kwa mara kwa kuwapelekea mahitaji mbalimbali ili kuwatia moyo kwenye

DKT. CHANA AIPONGEZA NPS KWA UTENDAJI KAZI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa  kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tarehe 02 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tarehe 02 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria kuongea na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tarehe 02 Novemba, 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) na kupokea tarifa ya utekelezaji ya mwaka wa fedha 2022/23 na kuipongeza kwa utekelezaji wa majukumu yake ya usimamiaji haki nchini. Dkt. Chana akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb), SACP Neema Mwanga aliyemwakilisha Katibu Mkuu amekutana na Menejimenti na watumishi wa ofisi ya
Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisoma Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria wa mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023), tarehe 31 Oktoba, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akimpongeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana baada ya kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria wa mwaka 2023, tarehe 31 Oktoba, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesoma kwa mara ya tatu Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria wa mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023) na kuridhiwa na Bunge na sasa utapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo naye akiridhia Muswada huo utakuwa sheria. Muswada huo unaolenga kufanyia marekebisho sheria Ish