DPP afuta Kesi 59 zaidi jijini Mbeya
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Chalya J. Nyangidu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Biswalo Mganga (wa pili kulia), walipotembelea Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya leo tarehe 28 Nov. 2019 wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa akiwatambulisha Staff wa gereza hilo mbele ya Waziri. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kulia akiwa na mwenyeji wake Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkoa wa Mbeya Mathias Mkama (ACP) katikati, alipotembelea Gereza Kuu la Ruanda Mbeya 27 Nov. 2019. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya Vendeline Tesha wakati wa ziara ya ki...