DKT. NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU WA KENYA
XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax katika Hafla ya maadhimisho ya miaka ya 58 ya Uhuru wa Taifa la Kenya yaliyofanyika tarehe 12/12/2022, Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana, Amidi wa Mabalozi wa mataifa mbalimbali Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui. Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya, ni fursa pekee ya kuangalia mahusiano baina ya nchi hizo mbili ambapo siku zote yamezidi kuimarika kama yalivyoasisiwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Aidha, Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa pamoja na kwamba mahusiano katika Nyanja za Biashara yamezidi kuimarika zinahitajika jitihada zaidi na kutoa rai kwa wafanyabiashara kue...