WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati Mhe. Waziri alipofika ofisini hapo kutoa salamu. xxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 23 Januari, 2025 amewasili Mkoani Kigoma na kukutana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, kwa ajili ya kushiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia utakaofanyika tarehe 24 Januari, 2025 Mkoani Kigoma. Akizungumza mara baada ya Mhe. Waziri kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya salamu, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amesema kuwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi anapata Haki na kwa wakati kupiti...