Posts

Showing posts from February, 2025

KASI YA ELIMU YA KUANDIKA NA KUTUNZA WOSIA IONGEZWE

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza kasi katika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza wosia pamoja na kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ya kijamii nchini. Wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoani Lindi, Waziri Mkuu pia amewaagiza wakuu wa wilaya kote nchini kuwatumia Mawakili wa serikali ngazi ya Wilaya, Halmashauri na Mikoa katika kuwa na programu mbalimbali za kusikiliza na kutatua kero za kisheria kwa wananchi ngazi ya Halamshauri. Wakati wa hotuba yake Waziri Mkuu pia amewahimiza Viongozi wa dini na Viongozi wa kimila kuendelea kuhubiri na kuhimiza kuhusu upendo, Mshikamano na maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kuendelea kutunza amani, umoja na mshikamano wa jamii. Waziri Mkuu Majaliwa ametumia fursa hiyo pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maam...

MSLAC INATEKELEZA FALSAFA YA 4R ZA RAIS SAMIA

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameitaja Kampeni ya kitaifa ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuwa ya kipekee, mahususi na inayotekeleza sharti la kisheria la kuwa na msaada wa kisheria kwa wananchi na yenye kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R yenye kuhimiza kuhusu maridhiano na ujenzi wa Tanzania mpya. Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo mjini Ruangwa mkoani Lindi mbele ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Kabudi amesema kwa Tanzania sharti la msaada wa kisheria limepanua wigo zaidi kwani linatoa msaada kwenye kesi zote ikiwemo zile za madai pamoja na jinai. Prof. Kabudi ameitaja wizara ya Katiba na Sheria kuwa mtekelezaji mkubwa na msimamizi wa falsafa hiyo ya Rais Samia Suluhu Hassan, akimshukuru pia kwa kuasisi kampeni hiyo pamoja na uwezeshaji wake mkubwa alioutoa kuwezesha kampeni hiyo kuwafikia watu wengi zaidi hasa ...

MSLAC IMESAIDIA KUKUZA UELEWA WA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KWA WANANCHI NA WATENDAJI

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxx Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdalah Sagini amesema Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imesaidia kukuza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa wananchi na watendaji wa serikali huku pia ikikuza na kuimarisha huduma za ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika wa vitendo mbalimbali ya kikatili. Mhe. Sagini amebainisha hayo Februari 19, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Lindi, akisema pia kampeni hiyo imesaidia kukuza imani kwa wananchi katika utatuzi wa migogoro mbalimbali kwa njia mbadala sambamba na kukuza uelewa wa watendaji wa serikali ngazi ya jamii kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sheria, utawala bora na utawala wa sheria kama nguzo kuu ya maendeleo, amani na utulivu wa nchi. Naibu Waziri Sagini pia amesema Kampeni hiyo kufikia Januari mwaka huu ilikuwa imezinduliwa kwenye mikoa 17 na Februari hii inazinduliwa na kutekelezwa kwenye mikoa mitano na mpango wa serikali ni kwamba kufikia mwezi Mei ...

WANASHERIA WA SAMIA WAMALIZA MGOGORO WA MAJIRANI MWANZA

Image
 xxxxxxxxxxxx Jopo la Wanasheria wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo Februari 19, 2025 Jijini Mwanza wamefanikiwa kutatua changamoto ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kata ya Nyamagana. Hayo ya yamejili kufuatia utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Jijini humo ambapo majirani hao Johanes Johnbosco na Bw. Yassin Suleiman walitofautiana kwenye matumizi ya ardhi. Imeelezwa kwamba Bw. Johanes aliingia makubaliano ya kuchimba na kujenga shimo la maji taka katika eneo la jirani yake huyo kupitia kwa mmiliki wa awali wa eneo hilo baada ya Bw. Johanes kukumbana na changamoto ya mwamba katika eneo lake. Hata hivyo shimo hilo limekuwa likitumiwa kwa pamoja na mmiliki wa awali hadi mmiliki wa sasa kabla ya kupishana na kumtaka Bw. Johanes kuacha kutumia shimo hilo Baada ya wanasheria hao kufika eneo la tukio wamefikia maridhiano kuwa kwa s...

WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA MSLAC LINDI WAPATIWA MAFUNZO

Image
  Mkurugenzi Idara ya Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi akizungumza na Wananchi wa Ruangwa Mkoani Lindi kupitia Redio Ruangwa ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia na kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria tarehe 19 Februari, 2025 Mkoani Lindi. xxxxxxxxxxxxxxx Wizara ya Katiba na Sheria imeendesha kikao cha mafunzo kwa Wataalam watakaoshiriki katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria Mkoani Lindi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) yenye lengo la kutoa elimu mbalimbali za Kisheria pamoja na utatuzi wa migogoro. Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bwana. Nathalis Linuma ametoa rai kwa washiriki wa kikao hicho kuzingatia na kutumia mafunzo hayo kama chachu na mwangaza wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapatia huduma za msaada wa kisheria katika kipindi cha kampeni. "Ni matarajio yangu kuwa mtafuata ...

TUMIENI SAMIA LEGAL AID KUTOA HAKI - RC MTANDA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akikagua banda la Wizara ya Katiba na Sheria alipowasili katika viwanja vya Furahisha kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025. Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Alfred Dede akitoa salamu za Wizara kwa Niaba ya Katibu Mkuu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025 Jijini Mwanza. Wananchi wa Mkoa wa Mwanza wakiwa  katika maandamano kuelekea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ikiwa ni Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya  Mama Samia Legal Aid tarehe 18 Februari,  2025 katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewasihi viongozi wa Mkoa huo kuendelea kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo ili kuwaletea wananchi hao Maendeleo. Mhe. Mtanda amesema hayo ...