Posts

Showing posts from 2025

UZINDUZI WA MSLAC KAGERA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa akiwasili katika Uwanja wa Uhuru (Mashujaa) Mkoani Kagera kwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia leo Aprili 14, 2025. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Uhuru (Mashujaa) Mkoani Kagera kwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia leo Aprili 14, 2025. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jasson Rwezimula akitoa Salaam za Wizara wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera. Tarehe 14 Aprili, 2025. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera tarehe 14 Aprili, 2025
Image
 xxxxxxxxxxxxxxxxxx Mama Samia Legal Aid Campaign Yaweka Kambi Arusha. Timu ya watoa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya "Mama Samia Legal Aid" imeweka kambi rasmi Machi 27, 2025 Jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa kuihudumia Jamii inayokabiliwa na uhitaji wa Msaada wa Kisheria. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewashauri watumishi wa Samia Legal Aid kuwa wasikivu na kutanguliza utu wanaposhughulikia kero za Wananchi, kwani wanamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni Wananchi kutatuliwa changamoto zao. "Mnatakiwa kuwa wasikivu na kutanguliza utu mnaposhughulikia kero za wananchi, kwani mnamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni wananchi kutatuliwa changamoto zao." Mhe. Makonda amesema hayo wakati akiongea na wataalam wa Sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwaaajili ya kupanga mikakati ya utatuzi wa cha...

WATENDAJI WA KATA KUWENI WAZALENDO KWA MASLAHI YA TAIFA

Image
  xxxxxxxx Watendaji wa kata wa Wilaya ya Mkinga wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuacha tabia ya kuwasaidia raia wa kigeni kupata vitambulisho bila kufuata taratibu za nchi kwa kuwa kufanya hivyo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa. Rai hiyo imetolewa na Afisa Tawala Mwandamizi Erick Farahani wakati alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Gilrbet Karima katika kufungua Mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa Kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata yanayoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria. “Sisi ndio tunaohusika kuwatambulisha wananchi, hii imekuwa ni changamoto kwetu sisi mpakani, mnapomtambulishi mtu kana kwamba yeye ana haki za uraia wa Tanzania tunawaomba kuwa wazalendo kweli” Kwa upande wake Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Adv. Dorice Dario amesema malengo ya kutoa elimu hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.

ASASI ZAIPONGEZA SERIKALI UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI.

Image
  Mkurugenzi Msaidizi wa Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Beatrice Mpembo, akiongea kwenye Kikao Kazi  kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mkataba  wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Itifaki ya Maputo. xxxxxxxxxxxxx Asasi za Kiraia na Haki za Binadamu zimeeleza kuridhishwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Itifaki ya Maputo. Pongezi hizo zimetolewa wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 19 hadi 21, 2025, ambapo wadau wamekutana na kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mkataba huo. Akizungumza katika kikao hicho Wakili Laetitia Ntagazwa, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amesema kuwa miongoni mwa mambo yanayosaidia katika kuimarisha Utawala wa Haki nchini ni pamoja na amani iliyopo jambo ambalo kila Mtanzania anapaswa kujivunia. Wakili Laetitia aliongezea kuwa licha ya Tanzania kumpoteza Kiongozi wa ...

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA MWANZA YAHIMIZWA UWAJIBIKAJI

Image
 xxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Machi 18, 2025 Jijini Mwanza   ameongoza kikao na watumishi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa   Mkoa huo ambapo amewahimiza umuhimu wa uwajibikaji katika kazi zao. Akizungumza katika   kikao hicho, Mhe. Ndumbaro amesisitiza kwamba ni muhimu kwa watumishi hao kuongeza ufanisi ili kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi na   kusaidia katika utoaji wa Haki kwa wananchi. Nae Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa huo Bw. Joseph Mahugo, amemthibitishia Waziri Ndumbaro kwamba ofisi yake itaendelea kutoa huduma bora kwa maslahi ya taifa. Ziara ya Waziri Ndumbaro Jijini Mwanza ina lengo la kufanya ukaguzi wa shughuli za ofisi hiyo na kuona jinsi wanavyoweza kuboresha huduma zao kwa umma.

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZINGATIENI SHERIA - KM MASWI

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg.Eliakim Maswi akizungumza na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)ambapo ametoa wito kwa wadau hao kuzingatia Sheria za Nchi na kufanya kazi kwa ushirikiano xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg. Eliakim Maswi ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kuhakikisha wanafuata sheria za nchi, taratibu zilizowekwa, na kufanya kazi kwa ushirikiano bila ubinafsi. Maswi ametoa wito huo Machi 18, 2025 jijini Dodoma, wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wanachama wapya wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC.) Amesema kuwa mashirika hayo yana nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya sheria zinazowasimamia, ili serikali iweze kufanya mabadiliko pale inapohitajika kwa ajili ya kuimarisha haki za binadamu kwa wananchi. Aidha, amewataka wanachama wapya wa THRDC kuwa mabalozi wa ha...

SIMAMIENI MALALAMIKO YA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU - DKT. MWANDAMBO

Image
  Watendaji wa Jiji la Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya Uraia na Utawala Bora yaliyofanyika tarehe 15 Machi, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Dkt. Stephen Mwandambo amewataka Watendaji wa Kata kusimamia malalamiko ya wananchi ya ukiukwaji wa Haki za Binadamu. Dkt. Mwandambo ameyasema hayo tarehe 15 Machi, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa Kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja  na Watendaji wa Kata wa Halmashauri ya Jiji la Tanga. “Mafunzo haya yatamsaidia Mkurugenzi kutoa nafuu kwenye utekelezaji wa  majukumu na tunategemea kuona  huduma zimeboreshwa katika ngazi zote baada ya mafunzo haya.“ Mwandambo amesema kupitia mafunzo waliyopata watatekeleza kwa vitendo na kuhakikisha falsafa ya “4R“ ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inasambaa kutoka katika ngazi za chini mpaka za juu za uong...

KAMATI ZA USALAMA ARUSHA ZATAKIWA KUFANYA KAZI KAMA TIMU

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa, Wawezeshaji   wa Mafunzo ya Utawala Bora na Urai mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya Uraia na Utawala Bora mafunzo   yanayoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki. Tarehe 13 Machi, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Paul Makonda, amewataka wajumbe wa Kamati za Usalama mkoani humo kufanya kazi kama timu, pamoja na kuwa na vipaumbele vya miradi ya kimkakati inayopaswa kujivunia kwa viongozi wa kitaifa wanapotembelea mkoa huo. Makonda amezungumza hayo wakati akifunga mafunzo ya elimu ya uraia na utawala bora kwa wajumbe wa Kamati ya Usalama wa Mkoa wa Arusha pamoja na kamati za usalama za Wilaya ya Arusha na Arumeru, yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, tarehe 13 Machi, 2025. Amesema Arusha kama mkoa unapaswa kuwa na mambo makubwa yanayoweza kufanywa kipaumbele kwa viongozi wa Kita...

MASWI AHIMIZA KUKAMILISHWA UJENZI WA JENGO LA WIZARA MTUMBA

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma. Tarehe 11 Machi, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxxx Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi amesema kuwa Wizara itaanza matumizi ya ofisi za jengo jipya ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake kwa kuhakikisha yeye mwenyewe akiwa ameambatana na timu ya Menejimenti inaanza kutumia jengo hilo ambalo mpaka sasa limefikia asilimia 86 ya ujenzi. Katibu Mkuu Maswi amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma Machi 11, 2025 huku akimhimiza Mkandarasi SUMA JKT Kanda ya Mashariki kuongeza kasi zaidi ili kuendana na makubaliano ya mkataba wa ukamilishaji wa jengo hilo. "katika kuendelea kuboresha utendaji kazi wa Wizara tumefanikiwa kupata Watumishi wapya na wapo Watumishi waliohamia hivyo uhitaji wa ofisi ni mkubwa sana. Nimeona ni vyema nianze mimi...

4RS ZA RAIS SAMIA ZAITIKISA GENEVA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushiriki katika Kikao cha 58 cha Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva Nchini Uswisi. 24 Februari, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxxxx Akizungumza  wakati akiiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Kikao cha 58 Cha Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva Nchini Uswisi tarehe 24 Februari, 2025 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa,   Nchi ya Tanzania imeendelea kuweka kipaumbele katika uendelezaji na ulinzi wa Haki za Binadamu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali. Waziri Ndumbaro amesema  kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984, Tanzania  imeendelea kusimamia Utu wa Kibinadamu kwa mujibu wa  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na inaendana na mkakati uliopitishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...

KASI YA ELIMU YA KUANDIKA NA KUTUNZA WOSIA IONGEZWE

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza kasi katika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza wosia pamoja na kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ya kijamii nchini. Wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoani Lindi, Waziri Mkuu pia amewaagiza wakuu wa wilaya kote nchini kuwatumia Mawakili wa serikali ngazi ya Wilaya, Halmashauri na Mikoa katika kuwa na programu mbalimbali za kusikiliza na kutatua kero za kisheria kwa wananchi ngazi ya Halamshauri. Wakati wa hotuba yake Waziri Mkuu pia amewahimiza Viongozi wa dini na Viongozi wa kimila kuendelea kuhubiri na kuhimiza kuhusu upendo, Mshikamano na maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kuendelea kutunza amani, umoja na mshikamano wa jamii. Waziri Mkuu Majaliwa ametumia fursa hiyo pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maam...

MSLAC INATEKELEZA FALSAFA YA 4R ZA RAIS SAMIA

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameitaja Kampeni ya kitaifa ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuwa ya kipekee, mahususi na inayotekeleza sharti la kisheria la kuwa na msaada wa kisheria kwa wananchi na yenye kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R yenye kuhimiza kuhusu maridhiano na ujenzi wa Tanzania mpya. Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo mjini Ruangwa mkoani Lindi mbele ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Kabudi amesema kwa Tanzania sharti la msaada wa kisheria limepanua wigo zaidi kwani linatoa msaada kwenye kesi zote ikiwemo zile za madai pamoja na jinai. Prof. Kabudi ameitaja wizara ya Katiba na Sheria kuwa mtekelezaji mkubwa na msimamizi wa falsafa hiyo ya Rais Samia Suluhu Hassan, akimshukuru pia kwa kuasisi kampeni hiyo pamoja na uwezeshaji wake mkubwa alioutoa kuwezesha kampeni hiyo kuwafikia watu wengi zaidi hasa ...

MSLAC IMESAIDIA KUKUZA UELEWA WA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KWA WANANCHI NA WATENDAJI

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxx Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdalah Sagini amesema Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imesaidia kukuza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa wananchi na watendaji wa serikali huku pia ikikuza na kuimarisha huduma za ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika wa vitendo mbalimbali ya kikatili. Mhe. Sagini amebainisha hayo Februari 19, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Lindi, akisema pia kampeni hiyo imesaidia kukuza imani kwa wananchi katika utatuzi wa migogoro mbalimbali kwa njia mbadala sambamba na kukuza uelewa wa watendaji wa serikali ngazi ya jamii kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sheria, utawala bora na utawala wa sheria kama nguzo kuu ya maendeleo, amani na utulivu wa nchi. Naibu Waziri Sagini pia amesema Kampeni hiyo kufikia Januari mwaka huu ilikuwa imezinduliwa kwenye mikoa 17 na Februari hii inazinduliwa na kutekelezwa kwenye mikoa mitano na mpango wa serikali ni kwamba kufikia mwezi Mei ...

WANASHERIA WA SAMIA WAMALIZA MGOGORO WA MAJIRANI MWANZA

Image
 xxxxxxxxxxxx Jopo la Wanasheria wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo Februari 19, 2025 Jijini Mwanza wamefanikiwa kutatua changamoto ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kata ya Nyamagana. Hayo ya yamejili kufuatia utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Jijini humo ambapo majirani hao Johanes Johnbosco na Bw. Yassin Suleiman walitofautiana kwenye matumizi ya ardhi. Imeelezwa kwamba Bw. Johanes aliingia makubaliano ya kuchimba na kujenga shimo la maji taka katika eneo la jirani yake huyo kupitia kwa mmiliki wa awali wa eneo hilo baada ya Bw. Johanes kukumbana na changamoto ya mwamba katika eneo lake. Hata hivyo shimo hilo limekuwa likitumiwa kwa pamoja na mmiliki wa awali hadi mmiliki wa sasa kabla ya kupishana na kumtaka Bw. Johanes kuacha kutumia shimo hilo Baada ya wanasheria hao kufika eneo la tukio wamefikia maridhiano kuwa kwa s...

WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA MSLAC LINDI WAPATIWA MAFUNZO

Image
  Mkurugenzi Idara ya Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi akizungumza na Wananchi wa Ruangwa Mkoani Lindi kupitia Redio Ruangwa ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia na kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria tarehe 19 Februari, 2025 Mkoani Lindi. xxxxxxxxxxxxxxx Wizara ya Katiba na Sheria imeendesha kikao cha mafunzo kwa Wataalam watakaoshiriki katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria Mkoani Lindi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) yenye lengo la kutoa elimu mbalimbali za Kisheria pamoja na utatuzi wa migogoro. Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bwana. Nathalis Linuma ametoa rai kwa washiriki wa kikao hicho kuzingatia na kutumia mafunzo hayo kama chachu na mwangaza wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapatia huduma za msaada wa kisheria katika kipindi cha kampeni. "Ni matarajio yangu kuwa mtafuata ...

TUMIENI SAMIA LEGAL AID KUTOA HAKI - RC MTANDA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akikagua banda la Wizara ya Katiba na Sheria alipowasili katika viwanja vya Furahisha kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025. Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Alfred Dede akitoa salamu za Wizara kwa Niaba ya Katibu Mkuu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025 Jijini Mwanza. Wananchi wa Mkoa wa Mwanza wakiwa  katika maandamano kuelekea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ikiwa ni Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya  Mama Samia Legal Aid tarehe 18 Februari,  2025 katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewasihi viongozi wa Mkoa huo kuendelea kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo ili kuwaletea wananchi hao Maendeleo. Mhe. Mtanda amesema hayo ...

WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji   Thobias Andengenye wakati Mhe. Waziri alipofika ofisini hapo kutoa salamu. xxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 23 Januari, 2025 amewasili Mkoani Kigoma na kukutana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji   Thobias Andengenye, kwa ajili ya kushiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia utakaofanyika tarehe 24 Januari, 2025 Mkoani Kigoma. Akizungumza mara baada ya Mhe. Waziri kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya salamu, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amesema kuwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi anapata Haki na kwa wakati kupiti...

WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA 100 MKOANI MTWARA WAPIGWA MSASA

Image
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bi. Bahati Geuzye akihutubia wakati akifungua kuanza kwa mafunzo ya Waratibu 100 wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid campaign) kutoka Halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara, tarehe 23 Januari, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxx Waratibu 100 wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid campaign) kutoka Halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara wamepatiwa mafunzo ya utekelezaji wa kampeni hiyo   kuelekea kuanza kwa utoaji huduma ya kisheria kwa wakazi wa mkoa huo ambayo yataanza Januari 24 hadi Februari 2, mwaka huu. Akiongea wakati wa kuzindua mafunzo hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bi. Bahati Geuzye amewataka waratibu hao kuhakikisha kwamba mafunzo wanayopatiwa kuhusiana na kampeni hiyo yanakuwa chachu na kuwawezesha kuwahudumia wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na uhitaji wa kupata huduma za msaada wa kisheria ili kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili. Bi. Geuzye amesisiti...

MAZOEZI YA UTIMAMU WA MWILI KUELEKEA UZINDUZI WA MSLAC KATIKA MIKOA SITA.

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi katikati akiongoza mazoezi ya utimamu wa mwili kwa baadhi ya wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo Januari 16, 2025 Mtumba Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika Mikoa Sita. Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na mazoezi ya viungo Januari 16, 2025 Mtumba Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria katia Mikoa sita.

WIZARA YAWAPIGA MSASA WARATIBU WA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

Image
  Wizara ya Katiba na Sheria imetoa mafunzo kwa Waratibu wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji   wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yameanza tarehe 14 Januari, 2025 katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani. Waratibu wa Mawakili wa Serikali, Wahadhiri Wasaidizi wa Vyuo Vikuu na Mawakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku mbili katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani, tarehe 14 Januari, 2025. xxxxxxxxxxxxxxxxxx Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) zinafikia Watanzania kwa ufanisi. Katika hatua ya kuimarisha utekelezaji wa kampeni hiyo, mafunzo maal...

VIJANA WATOA MSAADA WA KISHERIA WAMPONGEZA KM MASWI

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akipokea zawadi kutoka kwa Vijana watoa Msaada wa Kisheria waliojiunga na Wizara ya Katiba na Sheria miezi minne iliyopita kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Vijana hao wapatao 12 waliowakilishwa wameoneshwa kuguswa na utendaji kazi wa Katibu Mkuu na moyo wa kuwajali. T arehe 10 Januari, 2025 Mtumba, Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Ikiwa ni miezi minne tangu vijana wapatao 12 wenye taaluma ya Sheria walipojiunga na Wizara ya Katiba na Sheria na kushirikiana na Wataalamu wa Wizara katika mafunzo kwa vitendo vijana hao wameonesha kuguswa na kumkabidhi zawadi ya pongezi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Eliakim Maswi kwa utendaji kazi wake na moyo wa kuwajali. Wakizungumza mara baada ya kumtembelea Katibu Mkuu ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo tarehe 10 Januari, 2025 mwakilishi wa vijana hao  Prisila Kayuli amesema kuwa kwa kipindi chote wameshiriki na kupata ushirikiano ipasavyo katika shughuli mbalimbali za Wiza...

JAPAN KUSHIRIKIANA NA WIZARA KUENDELEZA SEKTA YA SHERIA NCHINI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na ugeni kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Yasushi Misawa wakati alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 8 Januari, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa alipomtembelea Mhe. Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa na Katibu Mkuu wa W...