Posts

Showing posts from July, 2024

NATAKA WATUMISHI WAWAJIBIKAJI – MASWI

Image
  Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Bw. Eliakim Chacha Maswi akiongea na Menejimenti na Watumishi wa Wizara kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma. Aliyekuwa Katibu Mkuu na sasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo akitoa neno la shukrani kwa Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi na Katibu Mkuu Eliakim Chacha Maswi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza wakati wa  hafla ya kumkaribisha Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma. Aliyekuwa Katibu Mkuu na sasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi nyaraka mbalimbali za Wizara wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma. Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Katiba na Sheria...

WAZIRI CHANA AONGOZA MAPOKEZI YA KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA

Image
Bwana Eliakim Chacha Maswi akila kiapo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Julai 26, 2024 Ikulu Dar es Salaam. Bwana Eliakim Chacha Maswi (mwenye shada la maua) baada ya kupokelewa na Viongozi wa Wizara na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Wizara, Julai 26, 2024 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana akiongea kwenye hafla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Maswi, Julai 26, 2024 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiongea kwenye hafla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Maswi, Julai 26, 2024 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dar es Salaam. Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi akiongea na Viongozi wa Wizara na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Wizara kwenye hafla ya kumpokea kama Katibu Mkuu mpya, Julai 26, 2024 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akieleze...

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maveterani waliopigana vita ya Uganda wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye Viwanja vya Mashujaa eneo la Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Julai 25, 2024.

WAZIRI DKT. PINDI CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SWITZERLAND

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Switzerland aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Bw. Didier Chasot. Julai 22, 2024 Dar es Salaam. Balozi wa Switzerland aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Bw. Didier Chasot akifanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana. Julai 22, 2024 Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Switzerland aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Bw. Didier Chasot kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maofisa kutoka ofisi hizo mbili baada ya kufanya mazungumzo. Julai 22, 2024 Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana leo Julai 22, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Switzerland nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Didier Chasot. Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, kililenga kujadili namna ya kuendeleza   mashirikiano katika kulinda h...

WATUMISHI WAPATA MFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI "RISK MANAGEMENT"

Image
  Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na mafunzo ya Usimamizi wa Vihatarishi "Risk Management," Julai 18, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Bi. Adolphina Lugendo kutoka Wizara ya Fedha.

WIZARA YAITA WADAU UBORESHAJI WA DAFTARI LA ORODHA YA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

Image
  Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi akiwasilisha rasimu ya daftari la orodha ya watoa huduma wa Msaada wa kisheria kwa wadau walioshiriki uboreshaji wa Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria. Julai 16, 2024 Dodoma. Mdau Maiko Salali kutoka asasi ya Foundation for Disability Hope akichangia katika mjadala wa kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria leo tarehe 16/07/2024. Leonard Haule ambaye anatokea TAKUKURU lakini pia ni mwakilishi wa Chama cha Mawakili wa Serikali akichangia katika mjadala wa kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria leo tarehe 16/07/2024. Baadhi ya wadau wa kikao cha kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria wakifuatilia wasilisho la rasimu ya daftari la orodha ya watoa huduma wa Msaada wa kisheria leo tarehe 16/07/2024 Mtumba Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxx Lusajo Mwakabuku – WyKS Dodoma. Wizara ya Katiba na Sheria leo tarehe 16/07...

UKAGUZI UNAONGEZA THAMANI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI - MAKONDO

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2023/2024, katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma, Julai 15, 2024. Msaidizi wa Mkaguzi  Mkuu wa Serikali Esnath Nicodem (wa kwanza kulia) akiwasilisha taarifa ya Kaguzi zitakazofanyika ambapo Kaguzi za hesabu za Serikali  za  Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2023/2024. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiongoza kikao kilichowahusisha Wakaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Timu ya Menejimenti ya Wizara  kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma, Julai 15, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima- WyKS Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amesema kuwa  kaguzi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Taasisi zake  zimewezesha kuboresha utoaji huduma na kuongeza thamani na ubora...

WOTE TUNA HAKI SAWA TUWAJALI WENYE MAHITAJI MAALUM – MAKONDO

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akisoma hotuba ya uzinduzi katika ukumbi wa American Corner uliopo Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria, Julai 12, 2024. Baadhi ya wajumbe na washiriki wa uzinduzi wa Mradi wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala kwa watu wenye ulemavu, Julai 12, 2024 Jijini Dar es salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akizindua rasmi Mradi wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala kwa watu wenye ulemavu, Julai 12, 2024 Dar es Salaam. Erick Mukiza, Mkurugenzi Mtendaji wa ESS Creative & Legal Foundation (ESS) akielezea malengo ya kuanzisha Mradi wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala kwa watu wenye ulemavu, Julai 12, 2024 Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Board ya ESS Creative & Legal Foundation (ESS) Dkt. Elly Ndyetabula akitoa salamu za ukaribisho kwa Mgeni Rasmi. Julai 12, 2024 Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WyKS Dar es salaam...

SAGINI AKOSHWA NA UBUNIFU WA MAHAKAMA KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao ambayo awali yalitanguliwa na  kutembelea jengo kuu la Mahakama ya Tanzania Tambukareli jijini Dodoma, Julai 11, 2024. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akimwelezea Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kuhusu utendaji kazi wa kituo cha huduma kwa mteja cha Mahakama kilichopo Tambukareli jijini Dodoma, Julai 11, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (Kulia), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa wamesimama mbele ya Ukumbi wa Mahakama namba mbili, ambao utatumika kwa ajili ya kusikiliza kesi mbalimbali pindi utakapomalizika. Julai 11, 2024 Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima, WyKS Dodoma Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Ju...

KAMATI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KIZAZI CHENYE USAWA

Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angella Kairuki akiongea kwenye kikao cha Kamati hiyo na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria, Julai 11, 2024 Mtumba, Dodoma. Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Mbaraka Stambuli akichangia hoja kwenye kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa, Julai 11, 2024 Mtumba, Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu Bi. Nkasori Sarakikya akiwasilisha taarifa ya Wizara juu ya jitihada zake za kuwezesha wanawake katika kufikia kizazi chenye usawa, Julai 11, 2024 Mtumba, Dodoma. Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara kwenye kikao na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa, Julai 11, 2024 Mtumba, Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Ch...

SAGINI AIPONGEZA MAHAKAMA KWA MSHIKAMANO

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza katika dua maalumu ya kumwombea marehemu  Amina Nyanda Juma ambaye ni mama mzazi wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma ambaye alizikwa Juni  Mosi, 2024, mkoani humo. Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha salaam za shukrani katika dua maalumu ya kumwombea marehemu  Amina Nyanda Juma ambaye ni mama mzazi wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma ambaye alizikwa Juni  Mosi, 2024, mkoani humo. Baadhi ya Wananchi, ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika dua ya kumwombea Amina Nyanda Juma ambaye ni mama mzazi wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma ambaye alizikwa Juni  Mosi, 2024 Tarime mkoani Mara xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima - WKS Naibu Waziri  wa  Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameipongeza Mahakama kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika utendaji kazi, majengo, matumizi ya TEHAMA, na k...

TATHMINI YA UKARABATI JENGO LA USULUHISHI IKAMILIKE KWA WAKATI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akiteta jambo na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walipotembelea jengo linalotarajiwa kutumika kama Kituo cha Usuluhishi lililopo Temeke,  jijini Dar es Salaam. Julai 6, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakitembelea jengo linalotarajiwa kutumika kama Kituo cha Usuluhishi lililopo Temeke,  jijini Dar es Salaam. Julai 6, 2024. xxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima – WKS Dar es Salaam Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Julai 6, 2024 akiwa ameambatana na baadhi ya Wakurugenzi  kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wametembelea katika jengo linalotarajiwa kutumika kuwa Kituo cha Usuluhishi kilichopo Temeke,  jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Sagini ameelekeza kuharakishwa kwa kazi ya kufanyika kwa  tathmini ya ukarabati wa jengo hilo inayofanywa na TBA ili...